Na.Mwandishi wetu
Umoja wa Mataifa kwa kupitia Shirika lake la wanawake leo umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani kwa kutoa wito kwa jamii kushirikiana kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake.
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam leo, Assistant Secretary-General, Deputy Executive Director for Policy and Programme wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa John Hendra amesema Umoja wa Mataifa unaunga mkono juhudi za Tanzania katika kukabiliana na ukiukwaji wa haki za mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla.
Awali akimkaribisha Bw. Hendra, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou amesema Umoja wa Mataifa unafanya kazi bega kwa began a serikali ya Tanzania katika kufanikisha utekelezaji wa sera ya haki na usawa kwa wanawake na wanaume.
|
Thursday, 8 March 2012
KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI LEO; UMOJA WA MATAIFA WAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPIGA VITA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment