Polisi wakiondoa mawe yaliyowekwa na wananchi sehemu walipogongwa wanafunzi hao. Leo majira ya saa nne asubuhi katika barabara ya kuelekea Hospitali ya Bugando imetokea ajali mbaya ya basi dogo la abiria (daladala) iliyokosa uelekeo na kusababisha vifo vya watoto wawili ambapo shuhuda amesema ““Hii gari ilikuwa inatiokea Bugarika inashuka kuelekea mjini, kwa spidi aliyokuwa nayo dereva kwa kweli ilikuwa hairidhishi kwani gari liliyumba kabla ya kufika Bar ya Bugando hill sisi tukalipisha tukakaa pembeni ilipofika karibu na Shule ya msingi Bugando dereva wa gari ikawa kama imemshinda akakwepa akaenda kugonga nguzo ya umeme akawa anahangaika kurudi barabarani eneo ambako kuna kama kivuko kwa wanafunzi ikamshinda na kupitia watoto wawili waliokuwa wakisubiri kuvuka barabara kisha akagota kwenye mawe yaliyopangwa pembezono” alisema Joseph Nyanda Karumbeti.Mtoto Elizabeth Kamsoka mwanafunzi wa darasa la 7 shule ya Msingi Sahara alifariki dunia papo hapo katika eneo la ajali mara baada ya kupasuka kichwa mazingira yanayotisha, nae Baraka Revocatus mwanafunzi wa darasa la 4 shule ya msingi Bugando amefariki dunia akiwa Hospitali ya Rufaa Bugando wakati juhudi za madaktari kuokoa maisha yake zilipogonga mwamba.
|
No comments:
Post a Comment