Tuesday, 11 September 2012
WANAHABARI MORO KUANDAMANA KESHO KULAANI MAUAJI YA DAUD MWANGOSI
Mratibu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro (MOROPC), Thadei Hafigwa.
WAKATI baadhi ya wanahabari wa mikoa ya Tanzania wameandamana leo kulaani mwenzao, Daud Mwangosi, kuuwawa na kitu kinachodhaniwa kuwa bomu kwenye mikutano ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) huko mkoani lringa, wanahabari wa mkoa wa Morogoro wameshindwa kuandamana leo baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kibali kitakachowaruhusu kufanya hivyo.
Akihojiwa na mwandishi wetu, mratibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (MOROPC) Thadei Hafigwa, alisema kwamba wamekwama baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kupata kibali hicho.
"Tunaandamana kesho kwa kukutana maeneo ya Posta ya mjini Morogoro hadi kwenye mzunguko wa barabara iendayo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na kuishia kwenye jengo la Shani Cinema. Tumeshindwa kufanya hivyo leo kwa kuwa sheria za kuomba kibali hicho inatakiwa kufanya hivyo kabla ya masaa 48," alisema Hafigwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment