WELCOME TO VIBES,FEEL FREE AND ENJOOY

Tuesday, 11 September 2012

Mwasiti apikwa na Mmarekani

MSANII nyota wa bongo fleva Mwasiti Almas ameamua kuuboreshja zaidi muziki wake kwa kutayarisha baadhi ya kazi zake na mtayarishaji mkubwa kutoka nchini Marekani anayekwenda kwa jina la Hakeem. Nyota huyo zao la kituo cha Tanzania House Of Talents (THT), alisema hivi karibuni kuwa pamoja na kuboresha, pia kufanya kwake kazi na mtayarishaji huyo ni katika kuleta ladha tofauti za muziki wake. Mwasiti ambaye kwa sasa anatamba na singo yake ya Mapito alisema tayari amesharekodi singo mbili chini ya Hakeem, hivyo anamini mashabiki wake watazipenda kazi zake hizo pindi atakapoziachia hewani. “Wimbo mmoja unazungumzia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanawake na nyingine ipo katika mtindo wa bongo fleva zaidi, nadhani mashabiki watazipenda”, alisema. Tangu achomoze katika tasnia ya bongo fleva, Mwasiti ameshatoa ‘singo’ kadhaa ambazo ziliweza kumuweka katika matawi ya juu ya chati za muziki katika vituo mbalimbali vya redio.

No comments:

Post a Comment