Tuesday, 11 September 2012
Mh. Lowassa akabidhi Madawati shule ya Msingi Minazi Mirefu,Kipawa jijini Dar leo
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi madawati yaliyotolewa na Kampuni ya African Barrick Gold kwa shule ya Msingi Minazi Mirefu,iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam leo.anaesaidiana nae ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikali wa Kampuni ya African Barrick Gold,Emmanuel Ole Naiko na aliesimama nyuma ya Mh. Lowassa ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Mh. Makongoro Mahanga
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati),Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga (kulia),Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikali wa Kampuni ya African Barrick Gold,Emmanuel Ole Naiko (pili kushoto) na Meneja Mawasiliano wa African Barrick Gold,Nector Pendaeli (kushoto) wakiwaangalia wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu,iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam leo waliokuwa wameketi kwenye sehemu ya Madawati 500 yaliyokabidhiwa leo na Kampuni ya African Barrick kwa shule hiyo.Hii ni sehemu ya Jitihada zinazofanywa na Diwani wa Kata ya Kipawa,Bi. Boma Kaluwa kwenye kuinua maendeleo ya kata yake.
Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh. Boma Kaluwa akizungumza machache mbele ya mgeni rasmi,wageni waalikwa na Wanafunzi wa Shule hiyo wakati wa hafla hiyo fupi ya kukabidhi madawati 500 kwa shule ya Msingi Minazi Mirefu,iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam leo.Mh. Kaluwa amekuwa akiwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kata yake inapata mafanikio makubwa hapa jijini kwa juhudi zake za kutafuta wafadhili mbali mbali ili waweze kumsaidia kuboresha maendeleo katika kata yake hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikari wa Kampuni ya African Barrick Gold, Emmanuel Ole-Naiko wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 500 katika Shule ya Msingi Minazi Mirefu iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimia na baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu,iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam leo wakiompokea kwa shangwe na bashasha tele.
Uongozi wa Kampuni ya African Barrick ukiwa katika picha ya Pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu,iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam leo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment