Thursday, 13 September 2012
BENKI INAYOFUATA SHERIA ZA KIISLAM YAPIGA HODI NCHINI UJERUMANI
nchini Ujerumani. Shirika hilo lina mpango wa kufanya hivyo mwezi wa kumi mwaka huu 2012 kwa matumaini kwamba athari mbaya zinazotokana na uchumi wa nchi za ulaya, zinaweza kupunguzwa na benki hizo ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa.
Muasisi na mkurugenzi wa Institute for Islamic Banking and Finance (IFIBAF) ndugu Zaid el- Mogaaddedi aliopo ktk mji wa Frankfurt nchini Ujerumani, alinukuliwa akisema ‘fikra nzima ya benki zinazofuata sheria za kiIslam ni kufuata maelekezo na kanuni za kiIslam.
Benki zinazofuata sheria za kiIslam zimeanzishwa nchi mbalimbali ktk bara la ulaya lakini wataalamu wa kiuchumi wamekadiria kwamba benki hiyo inaweza kufanikiwa sana nchini Ujerumani kuliko ilivyofanikiwa nchini Ufaransa na uingereza. Changamoto kubwa ni ile inayohusiana na uwezo wa benki za kiIslam kua na miundombinu na huduma nzuri alisema El-Mogaddedi.
Ujerumani ina idadi ya Waislam milioni 3, 8 hadi 4,3 ambao ni sawa na asilimia tano ukilinganisha na idadi ya wakazi wa Ujerumani ambao idadi yao ni milioni 82. Benki hiyo inawalenga waislam na wasiokua waislam. Uchumi unaofuata sheria za kiIslamu ni ktk moja ya uchumi ambao unakua kwa haraka sana duniani. Ktk jumla ya sababu za kukua kwa uchumi huo, ni pamoja na Waarabu kuondoa pesa zao nchini marekani na kuziweka ktk nchi za kiIslam ikiwemo Malysia na bara Arabu, baada ya uvamizi maarufu unaojulikana kama 9/11, ikifuatiwa na uchumi huo kuingiza faida ktk kipindi ambacho uchumi wa dunia ulitetereka. Kwa maelezo zaidi kuhusu uchumi na benki zinazofuata sheria za kiIslamu
Kwa info zaidi tembelea http://ijuebankyakiislam.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment