Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya watoto milioni 1.5 wako kwenye hatari ya kufa njaa kwenye eneo la Sahel Magharibi mwa Afrika.
UNICEF inasema kuwa mzozo uliopo pamoja na ukame huenda vikawa na madhara makubwa kwa maisha ya watoto walio chini ya miaka mitano.
Linasema kuwa lina mipango ya kuwalisha watoto miloni sita wanaosumbuliwa na utapiamlo kwa muda wa miezi sita inayokuja.
Marixie Maecado kutoka UNICEF anasema kuwa hali ya watoto kwenye eneo la Sahel ni kutokana na ukosefu wa ufadhili.
|
No comments:
Post a Comment