Kocha wa muda wa club ya soka ya Chelsea Roberto Di Matteo, amekiri kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Ferando Torres ana tatizo la kisaikolojia ambalo ndio linachangia kwa kiasi kikubwa mchezaji huyo kushindwa kufunga magoli.
Torres ambaye Chelsea ilimsajili akitokea Liverpool kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 50 na kwa muda wa mwaka mzima amefunga magoli matano pekee tu toka ajiunge na chelsea.
Sasa leo Di matteo amesema kuwa anaelewa kinachomsibu Torres ni presha kubwa aliyo nayo inayomfanya achanganyikiwe na kushindwa kufikira kama ilivyo kawaida yake anapokuwa kwenye eneo la hatari.
Di matteo hana presha na torres, na anasema anapaswa kutofikiria sana kuhusu kufunga bali awaze kucheza soka tu kwani kuna wakati utafika na atarudi kwenye hali yake ya kawaida ya kufunga magoli.
|
No comments:
Post a Comment