WELCOME TO VIBES,FEEL FREE AND ENJOOY

Monday, 10 September 2012

WAFUNGUKA KUHUSIANA NA KIINGEREZA KAMA KINACHANGIA UKUAJI WA MUZIKI NCHINI

Muziki ni hisia ndio maana hata baadhi ya watu wanapenda miziki ya kihindi au kilatini bila kujua maana kutokana na hisia zao kutekwa na jinsi waimbaji walivyowasilisha hisia kupitia muziki. Hivyo mie nadhani lugha sio tatizo kubwa kwa muziki wetu kuweza kwenda level ya kimataifa, tunachohitaji ni kuwa utambulisho wa muziki wa kitanzania ambao msanii yoyote haijalishi awe anachana au kuimba akitoa tu ngoma yake ijulikane hii ni kutoka Tanzania.
AFANDE

Language sio kigezo kabisa kwani muziki wa kizaire umefika mbali sana na hakuna anaelewa. So ni ubunifu na wasanii na maproducer kuwa serious kufanya muziki uwe biashara. Then kila kitu kitakuwa poa na international market itakuwa real, mbona Diamond, Kiba wanapiga show na hiki hiki kiswahili na wanakubalika.
MARCO CHALI

Tatizo sio language ni uvivu wa kuumiza kichwa wasanii wengi wanataka kutumia kivuli cha wasanii wengine. Kila anayekuja sasa hivi anataka kutambaa mwendo wa msanii flani, nadhani ndiyo kikwazo kikubwa cha mziki wetu kutokufika mbali.
MANECKY

No comments:

Post a Comment