Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika ukumbi wa MNelum Pokuna Mahinda Rajapaksa kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofunguliwa leo na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa,aliye pembeni yake ni Mjumbe wa CPA Tawi la Tanzania na Mbunge wa Kigoma Mhe. Zitto Kabwe
Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa akihutubia Maspika, Wabunge na maafisa zaidi ya 850 kutoka Mabunge ya nchi wanachama jumuiya ya madoloa wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano huo.
Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akifuatilia kwa umakini ratiba ya ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) kabla ya ufunguzi rasmi leo Mjini Colombo Sri, Lanka, aliye kushoto kwake ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho na Mhe. Zitto Kabwe na aliye kulia ni Mhe. Mussa Azzan Zungu
Wajumbe wote wa Mkutano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi leo.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
No comments:
Post a Comment