Tuesday, 11 September 2012
Lady Gaga ahudhuria party na mavazi ya Bibi Harusi
Picha hii isikuchanganye. Lady Gaga hakuolewa siku ya Jumapili bali aliamua tu kutoka kivyake kwa kuvaa shela kama bibi harusi kwenye party jijini London.
Gaga, akiwa na Jay-Z na Rihanna, walisababisha shangwe kubwa baada ya wote kuhudhuria kwenye sherehe za baada ya michezo ya Paralympic Games kwenye klabu ya Arts, ya London, Uingereza.
Gaga kama kawaida yake aliwashangaza wengi, baada ya kutoka kwenye gari akiwa na muonekano wa bibi harusi wakati Rihanna aliamua kutoka simple tu kwa kupiga pajama nyekekundu na jaketi la ngozi.
Mapema usiku huo, Rihanna aliungana na washkaji zake wa kundi la Coldplay na kuangusha bonge la performance wakati wa ufungwaji wa Paralympic Games.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment