Thursday, 13 September 2012
‘BABY BOY’ AONGELEA SABABU ZA UKIMYA WAKE KWENYE GEMU…!!
MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye aliwahi kutamba na ngoma kadhaa kali, Edson Wilson ‘Baby Boy’, amefunguka na kuuambia mtandao wa DarTalk, kuwa kisa cha ukimya wake ni kuwa yupo katika mchakato wa kutafuta menejimenti ambayo itamsaidia kusimamia na kuendesha kazi zake zote za muziki.
Awali kabisa msanii huyo alikuwa chini ya Zizzou Entertainment, ambao walikuwa wanaendesha kazi zake, lakini baada ya kuvunja mkataba na Zizzou hakuna kazi yoyote ya muziki aliyoitoa kitu ambacho kinafanya mashabiki wake wamkose.
Akiongea na DarTalk alidai kuwa bado anaendelea kufanya muziki lakini kikubwa kilichomweka kimya ni ishu hiyo kwani hawezi kufanya muziki mwenyewe bila usimamizi wa mtu wa watu, anaamini nguvu ya watu wengi ndiyo inayoleta maendeleo na kutimiza ndoto.
“Nimekuwa kimya kweli, hivi sasa natafuta menejimenti ambayo itakuwa itaendesha kazi zangu na kunifikisha pale nipopataka,” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa bado hajapata menejimenti lakini kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kuachoa ngoma kibao ambazo zipo studio ili mashabiki wake waweze kupata ujio wake mpya kabisa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment