Saturday, 2 February 2013
SEXIEST GIRL, BACHELOR… NGOMA INOGILE!
YALE mashindano yaliyojizolea umaarufu mkubwa kwenye magazeti Pendwa, Sexiest Girl na Sexiest Bachelor yamerejea upya kwa mwaka 2013, tayari waandaaji wameanza kuratibu majina.
Sexiest Bachelor 2009, Yusuph Mlela.
Kwa mujibu wa waandaaji, mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi hivi karibuni na sasa wapo katika mchakato wa kuchanganua vigezo vya washiriki ambao wamependekezwa katika hatua ya awali.
“Mwaka huu tunataka kuboresha zaidi mashindano yetu, tunachambua kwa makini ili kuwapata washiriki ambao watakuwa na vigezo vyote vinavyohitajika.“Mashabiki wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu tutaanza kuwaweka hadharani washiriki na wao wataanza kuwapigia kura ili mwisho tuwapate washindi", alisema Amran Kaima, mmoja wa waratibu.
Sexiest Girl 2012, Jacqueline Wolper.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment