Wednesday, 6 February 2013
FLAVIANA MATATA FOR DIESEL + EDUN
In January 2012, Diesel founder Renzo Rosso and EDUN founders Ali Hewson and Bono travelled to Uganda and Mali, where they shared their love of the continent and toured each other's programs: Diesel's Only The Brave Foundation project in Dioro, Mali and EDUN's Conservation Cotton Initiative (CCI) in Uganda. The experience was the catalyst for them to join forces to further apparel trade and development in Africa with a co-branded, co-designed collection.
COLLECTION IN-STORE AND ONLINE MARCH 2013
Mwanamitindo wa kimataifa kutoka nchini Tanzania Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESELna EDUN. Kampeni hiyo inayoitwa DIESEL + EDUN ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo muanzilishi wa kampuni ya DIESEL - Renzo Rosso - na waanzalishi wa kampuni ya EDUN - Ali Hewson na Bono walisafiri nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima wa pamba barani Africa. Waliingia makubaliano ya kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba ya wakulima hawa wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo basi nguo hizi zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.
Nguo hizo zitaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka mbalimbali nchini Marekani na duniani. Pia nguo za DIESEL + EDUN zitauzwa kupitia mitandao mbalimbali.
Mwanamitindo Flaviana Matata ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania 2007 anabaki kuwa mwanamitindo pekee kutoka bara la Africa katika kushiriki katika kampeni za nguo hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment