WELCOME TO VIBES,FEEL FREE AND ENJOOY

Wednesday, 5 September 2012

WEUSI – HIMAYA MPYA YA HIP HOP

Miaka takribani 10 iliyopita walikuwa wakisafiri 636 kilometres from Geneva of Africa-Arusha to the “harbour of peace” – Dar es Salaam, wakiwa hawana sehemu maalum ya kufikia katika harakati zao kutafuta namna ya kutengeneza himaya yao ndani Tzee music industry. Now, after a decade, they are now arguably the best Hip Hop group in Tzee music cycle with best rappers to ever grace the mic katika historia ya muziki wa kizazi kipya. Wakiwakilisha mjumuiko wa makundi mawili, River Camp Soldiers and Nako 2 Nako Soldiers, John Simon alias Joh Makini, Nickson Simon aka Nikki wa Pili, Godfrey Nyahongo aka Maarifa/Bonta, Isaack Waziri aka Lord Eyez and George Sixtus Mdemu aka G Nako, marafiki wa tangu utotoni na ndugu waliokulia eneo la Daraja mbili – Arusha, kwa pamoja baada ya kufanikiwa ku-establish himaya yao ndani ya music industry, now wameamua kwenda an extra mile katika kufanya muziki wao kuwa kibiashara kwa asilimia 100. They have officially formed a legally registered music company goez by tha name of “Weusi Company“, wakitaka kuhakikisha kazi zao zinafanikiwa na kuwawezesha kuishi vizuri kupitia jasho lao wanalovuja kwenye biashara ya muziki. Baabkubwa Magazine brings to you exclusive interview na shareholders wa kampuni ya kwanza inayoundwa na Hip Hop artists na iliyosajiliwa kisheria, huku wakiongelea kiundani kuhusu historia, malengo, na muelekeo wa “Weusi Company“. WEUSI COMPANY Kiafrika linapokuja suala la rangi wengi wetu ni weusi, ila kwa upande mwingine kwenye Tzee entertainment industry WEUSI is something deep, “Kwa wale wafuatiliaji wa ngoma za Joh Makini au Lord Eyez kwenye ngoma zao nyingi wakidai ni nyeusi kwa maana ya kwamba zimepatiwa. So mtu mweusi au kitu cheusi siku zote yaamananisha ni kikali” “When we talk of WEUSI COMPANY is the entertainment company inayojumisha muunganiko wa share holders watano kutoka N2N Soldiers na River Camp ambao ni Joh Makini, Lord Eyez, Bonta, Nick wa Pili na G-Nacko yenye lengo la ku-support kazi za wamiliki wake na pia kufanya kazi na watu wengine ambao so share holders ndani ya kampuni hii” – Bonta. BK: How did WEUSI COMPANY started? “As we told you earlier Weusi ni kampuni inayounganisha makundi yanayotoka katika dunia moja, bara moja, nchi moja, mkoa mmoja na kitongoji kimoja. Ni watu ambao tumekutana miaka mingi iliyopita tukiwa kama ndugu, hivyo muziki ulitukuta tayari tukiwa marafiki. Kwa wasiojua mara nyingi wasanii wa makundi haya mawili tulikuwa tukisafiri toka hometown kuja Dar kwa ajili ya shughuli za muziki where by we used kupanda gari moja most of the time na hata kushare maghetto tuliyokuwa tukikaribishwa kufikia hapa jijini, lakini tukawa tunatofautiana interms of brands linapokuja suala la kuingia studio kufanya kazi za crew. In addition to that, founders wote wa kampuni hii have been raised kwenye hood moja toka Arusha, tumekuwa marafiki kwanza tangu tukiwa wadogo kabisa, so we are brothers. Following this tukaamua kwa pamoja kuanzisha kitu ambacho kitatuweka kwa ukaribu na kuweza kutuunganisha zaidi ili kuweza ku-share common interests and thats where WEUSI COMPANY started“-added Bonta BK: Weusi Company inaongozwa na misingi na taratibu zipi? “Weusi ni kampuni inayotambulika kisheria kabisa, hivyo tunaongozwa na kitu kinachoitwa memorandum, kitu ambacho ndio kinachotoa muongozo wa namna gani sisi tunapaswa kufanya kazi na kuishi pamoja. Ni kitu ambacho ni kama katiba yetu.” – Bonta “Pia hii kitu tumeamua kuiweka kutokana kasoro za kibinadamu tulizonazo, lakini sisi tulianza kuwa kampuni kabla ya Weusi, sie ni familia moja hivyo tungeweza kuishi kama familia lakini kutokana na ukosefu wa kukamilika kibinadamu inabidi tuwe na vitu kama hivi vya kutuongoza.” – Joh Makini. BK: What does it takes kwa mtu kuweza kujiunga na Weusi? “Hii ni kampuni ya kibiashara, hivyo ikiwa kuna mtu anahitaji kujiunga na kampuni yetu milango ipo wazi. Kitu anachohitaji kufanya ni kununua shares ili aweze ku-qualify kuingia kwenye kampuni yetu.” BK: Does that mean mtu ambaye ana kipaji pekee hawezi kuwemo ndani ya Weusi Company? “Kwa mtu kipaji itabidi ajiunge na kundi moja kati ya Nako au River Camp ikiwa atafuzu vigezo vya member wa makundi hayo. Hawezi kuwa ndani ya Weusi kwa sababu hii ni kampuni inayoundwa na share holders tu.” MALENGO NA SABABU. BK: Ni sababu zipi zilizowasukuma kuunda kampuni hii?. “Sababu kubwa iliyotufanya tuweze kufanya kazi rasmi kama kampuni ni kuweza kuunda umoja wa kisheria uliotokana urafiki wa dhati kuweza kusogeza kazi zetu za kimuziki mbele zaidi na kuweza kufanikiwa. Kwa sababu umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu, pia tukiwa na umoja huu wa kisheria ni rahisi hata kuweza kupata misaada kutoka serikalini au kampuni binafsi kwa sababu inakuwa sauti ya wengi hivyo ni rahisi kusikilizwa shida zetu.”BK:Siku zote kila kitu ni lazima kiwe na lengo kuu, ni nini malengo ya kampuni hii? “Lengo letu kubwa wakati tunaanzisha WEUSI ni kuwa kila member/shareholder aweze kuwa na uwezo wa kujitegemea, kila mtu aweze kusimama as a brand inayojitegemea na pia watu wote watakaopitia chini ya kampuni hii waweze kujitegemea nikimaanisha kumuwezesha kila shareholder kuwa na maisha bora. “Pia malengo yetu mengine ni kufanya biashara nyinginezo kupitia muziki wetu. Kwa sasa tumeanza na kufungua clothing line yetu ambayo tayari tumeanza kwa kutoa Tshirts na top za kike zenye logo Weusi. Pia kwa sasa tupo locotion tuki-shoot kipindi chetu cha TV goez by the name of “Muda wa Weusi”, huku tukiwa katika hatua za mwisho kuweza kufungua our own recording studio, before hatujapiga extra step na kuweza kufungua radio station yetu. Vitu hivi vyote vitakuwa chini ya Weusi Company.” – Joh Makini. BK: Mnaonekana kuwa mipango mizuri na endelevu, lakini mtawezaje kufanikisha mipango yenu ikizingatiwa fedha nyingi inahitajika ili kufanikiwa? “Tunatambua ugumu uliopo katika kufanikisha mpango yetu yote, lakini tumejipanga vizuri, tuna na uwezo na nia thabiti katika kuhakikisha plans zetu haziwi ndoto za kusadikika. Tayari tupo kwenye mazungumzo na wadau kadhaa wa kiabiashara ambao tunaamini kama mambo yakienda sawa hatotukwama. Pia lazima mkumbuke sie wenyewe tayari tuna vipaji vikubwa ambavyo ndio mtaji wetu. Tunavitumia kama njia ya kuingizia income ambayo itasaidia kufanya mambo mengine. Tunaamini kwa baraka za mungu, mipango yetu ambayo tayari tumejiwekea muda wa kuitimiza itatimia. In God we trust”. MATATIZO NA CHANGAMOTO Historia inaonyesha kwamba miunganiko mingi ya wasanii hapa Tanzania imekuwa haidumu, haijalishi ni group au kampuni, itafikia mahali tu watakarofishana na kutokea kwa mvunjiko kati yao. Je Weusi Company imejipanga vipi kuweza kuepuka suala hili? “As we said earlier, sie tulianza kuwa marafiki tangu tukiwa watoto, muziki ulitukuta tayari tukiwa marafiki. Members wote wa Weusi hatukukutana kibiashara nikimaanisha kimaslahi, makundi mengi yaliyovunjika yalikutana kimaslahi, na pale biashara inapoyumba basi yana-collapse.” – Bonta. “Pia kitu kingine kinachosababisha makundi ama kampuni ni wanachama wa kundi/kampuni hiyo kushindwa kusimama individually, kitu ambacho lazima kilete utegemezi kwa mtu au watu ndani kampuni. That’s why Weusi tuna sera yetu ya kuhakikisha kila mmoja wetu anaweza kusimama kama brand inayojitegemea, ndivyo ambavyo tunaweza kuendelea bila kutokea kulumbana kwa misingi ya kimaslahi.” – Joh makini. BK: Changamoto gani mnazokumbana nazo? JOH: Challenge kubwa ambayo inaya-face makundi mengi ni kupata watu wenye kujuana kikazi na pia kitabia, kwetu sisi hii iko fresh, kama ambavyo tumesema tumejuana tangu utotoni hivyo tunafahamiana kitabia japokuwa kuna kasoro chache za kibidamu ambazo tunarekebishana kupitia kupitia katiba yetu. Changamoto kubwa zaidi tuliyonayo sasa hivi ni namna tunavyoweza kufanya kazi zetu za kila siku tukiwa hatuna financial support zaidi ya kile tunachotengeneza wenyewe. Tatizo lingine ambalo tunakutana nalo ni ushirikiano mdogo tunaopata kutoka kwa baadhi ya wasanii wenzetu in the music industry. Matatizo mengine ni yale ambayo kila mtu anayefanya biashara hii ya muziki au sanaa kwa ujumla anakutana nayo. Lakini tunaamini hizi changamoto ndio zinazotu-motivate kufanya kazi zetu kwa ubora zaidi.” MAFANIKIO Nearly a year tangu kampuni hii kuundwa, Weusi wamepata mafanikio mpaka kufikia sasa? “Mafanikio ya kwanza tuliyoyapata kwanza ni kuweza kuisimamisha kampuni hii. Ryt now kampuni inafanya kazi zake kisheria kabisa. Pili ni ile hali ya kuweza kuwa pamoja bila mizozo isiyokuwa na msingi wala maana yoyote, jambo hili kwetu ni mafanikio tayari. – G.Nako. ” Musically sasa hivi member yoyote wa Weusi Co. hatokuwa akitoa ngoma ambayo itakuwa na mapungufu kwa sababu tumejiwekea utaratibu mzuri wa kila mmoja wetu kuandika mashairi mazuri yaliyo ndani ya misingi ya Hip Hop. Kwa mfano jinsi ambazo sasa naandika ngoma zangu ni tofauti na zamani, rite now kila mstari ninaoandika unakuwa umekubalika na kusahihishwa na wenzangu wote, hivyo mwisho wa siku nafanya kitu bora. That’s why from now on hautasikia wimbo wowte wa kawaida kutoka kwa mwanachama yoyote wa Weusi. Huku ni kufanikiwa.” - Joh.Makini. “We thanks God kwamba kwa kumwamini yeye kama tulivyoeleza kwenye ngoma yetu ya pamoja ya “Watoto Wa Mungu” tumeweza kutengeneza album yetu ya kwanza chini ya kampuni hii itakayoitwa “Muziki Mzuri” which will be packed with 20 songs zenye collabos za wasanii kibao kama Nazizi, Ambrose, Farida, Kalamashaka, Belle 9, Ray C na Pipi. We are happy to inform fans wa brand hii ya Mziki Mzuri kuwa debut album hii ya WEUSI yenye touches za producers mbalimbali kama P.Funk, Dunga, Marco Chali, Lamar, Nareel, Q Tha Don, Fundi Samwel na wengine wengi kuwa iko kwenye hatua za mwisho mwisho ikikamilika ni mwendo wa kupata muziki mzuri“-Lord Eyez. WATOTO WA MUNGU MUSIC TOUR. Katika kujitambulisha rasmi kwa mashabiki wa muziki mzuri pamoja na kuitambulisha rasmi albam yao, Weusi wanatarajia kuanza kufanya tour ya karibia nchi nzima. “Tumeamua kufanya tour hii hili kuweza kujitangaza rasmi kwa mashabiki wetu. Pia tutakuwa tunazindua albam yetu ya “Muziki Mzuri”. Tour tunategemea itaanza in April, mikoa ambayo tutaenda ni Arusha, Iringa, Mbeya, Moshi, Mwanza, Morogoro, Shinyanga, Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma na kama mungu akijaalia mipango ikienda kama tunavyojaribu kuipanga iwe then tutaenda na visiwani Pemba na Unguja. Albam yetu tayari imeshatoka na tunaiuza wenyewe baada ya wadosi kutuzingua sana.” MUSIC INDUSTRY Katika miaka ya hivi karibuni unapozungumzia muziki wa Hip Hop basi kamwe huwezi kuacha kuyazungumzia makundi mawili kutoka A City, Nako 2 Nako Soldiers and River Camp. They have countless hits na kufanya vizuri katika vizuri shows mbalimbali huku wakishea one stage with some of the biggest artist on earth such as Jay Z, Ja Rule, 50 Cents, Busta Rhymes and Ludacris. Kwa pamoja as Weusi tayari wameshateka soko la muziki wa Hip Hop in Tzee, je wana plans zipi za kuweza kujitangaza kimataifa? “Mikakati tuliyojiwekea kutoka sasa ni kufanya muziki wenye ubora wa kimataifa, ambao utakidhi viwango vya kupigwa katika radio au TV station yoyote duniani. Tukifanikisha hilo tunaamini muziki mzuri wa “Watoto wa Mungu” utasambaa kama kansa mwilini. Pia tuna mipango thabiti ya kuweza kujitangaza kimataifa, inshallah ndani ya miaka miwili ijayo tutakuwa moja ya wasanii wakubwa Afrika.” Wasanii wengi wa muziki now dayz wamegoma kutoa albam kutokana na matatizo ya mfumo mbovu wa soko. Weusi mmeamua kutoa albam, je mmejipanga kuisambaza vipi ukizingatia mfumo huu mbovu tulionao katika soko la muziki Tanzania? “Albam yetu ya “Muziki Mzuri” tumeamua tutaisambaza wenyewe, kupitia tour yetu ya muziki tunajipanga kutafuta mabalozi wa watakaokuwa wakituwakilisha katika shule za sekondari na vyuo Tanzania nzima. Hawa mabalozi watakuwa na kazi ya kusambaza kazi zetu na products zote zinatoka Weusi Company. Tumeamua kufanya hivi kwa kuwa mfumo wa soko la muziki wa kibongo ni mbovu, ni ngumu sana kwa msanii kupata kile anachostahili. Sasa ni bora tusukume kazi zetu wenyewe kupitia mabalozi wetu, online na pia kwa kuuza products zetu katika shows tutakazokuwa tunafanya. “Cosota na sheria za hakimiliki hapa Bongo ndio zinazofanya sanaa ya Tanzania kutengeneza masikini wenye makubwa. Hivyo Weusi hatutaki na tumekataa kuwa watu namna hiyo.” Muziki wa Hip Hop unazidi kupata changamoto mpya kila siku. Wasanii wengi wakali wanaongezeka katika game. Weusi mmejipanga vipi kuweza kuhimili ushindani uliopo? “Kwanza kabisa tungependa kuweka wazi kwamba Weusi tunamuheshimu kila msanii anayefanya kazi nzuri, tunaona ujio wa wasanii wengi wenye vipaji lakini tunaamini bado tutaendelea kuwa namba moja na wapinzani watasubiri sana kutushusha, tumefunga ndoa ya milele na hii hip hop game. Wapinzani wa Weusi katika huu muziki ni sisi wenyewe, na kama radio station na TV zitataka kupiga muziki mkali basi nafikiri kuna watu itabidi waache kurap. Tumeirudisha Hip Hop Nyumbani.” – Joh.Makini.

No comments:

Post a Comment