WELCOME TO VIBES,FEEL FREE AND ENJOOY

Sunday, 9 September 2012

King Majuto kustaafu uigizaji

Utakataa tukimuita ‘mchekeshaji mahiri wa maisha yote’ (Best comedian of all time)? Ni ngumu kubisha. Amekuwa kwenye game kwa kipindi kirefu lakini ameendelea kuwa relevant! Hachoshi na hadi umri wake wa leo, anaweza kuzivunja mbavu zako kwa vituko vyake. Si mwingine, ni Amri Athumani maarufu kama King Majuto. Bad news kwa mashabiki wake ni kwamba November mwaka huu atastaafu shughuli za uigizaji. Sababu ya kustaafu anasema ni kutokana na umri wake kuwa mkubwa hivyo anaona ni vyema akiwaachia vijana waliendeleza libeneke! Hata hivyo hatopotea kabisa, kwakuwa ana mpango wa kugawa ujuzi kwa damu changa itakayopenda kupata muongozo wake.

No comments:

Post a Comment