WELCOME TO VIBES,FEEL FREE AND ENJOOY

Saturday, 8 September 2012

BAMBOO NA FRASHA ,KUNA BEEF ?

Week Mbili zilizopita yalifanyika mashindano ya Freestyle Kupitia Nokia Dont Break The Beat na palikuwa na wasanii tofauti waliopewa mualiko wa kufanya show kwenye mashindano hayo. Kati ya wasani hao P Unit, Bamboo walikuwepo na Bamboo alipandishwa kwenye stage na member wa Kundi la P Unit ,Frasha king wa Flow nchini kenya ambaye pia alikuwa Mshereheshaji wa mashindano hayo . Bamboo alifanya show ndefu na nzuri kwa watazamaji ,kila baada ya wimbo mmoja alitoa Freestyle alafu aliendelea na wimbo mwingine .Inasemekana P Unit ndio kundi lililofata kwenye stage baada ya Rapper Bamboo kushuka . Story ya Beef imeibuka baada ya watu waliokuwa kwenye show hio kusema kuwa Frasha hakutoa muda wa kutosha kwa Bamboo kumalizia show yake. Inasemekana maneno ya Frasha yalikuwa haya wakati Bamboo anashuka kwenye jukwa ' Hatujaja Hapa Kutambulisha Album ' . Baada ya Bamboo kusikia hivyo sura yake ilibadilika na kuonekana kama hajafurahishwa na maneno ya Rapper Frasha. Baada ya uvumi huu Manager wa Bamboo amekanusha habari za Beef nakusema Frasha na Bamboo wako Powa kabisa.

No comments:

Post a Comment