WELCOME TO VIBES,FEEL FREE AND ENJOOY

Tuesday, 24 April 2012

RAKIM ASEMA WASANII KAMA KANYE WEST WANAITAJIKA KATIKA MUZIKI WA HIP HOP

Akiwa katika game la Hip Hop kwa miaka 25 emcee Rakim, wasanii na mashabiki wamempa heshima kubwa emcee huyo kwa sanaa yake. Mwana Hip Hop amempa sifa nyingi Kanye West. Katika mahojiano na “The Atlantic” The God emcee huyo amemsifu sana Kanye West kwa licha tu ya kuwa rapper pia ni memba wa jamii ya hip hop, Alisema kama emcee na mtayarishaji wa mapigo ya muziki ameipeleka hip hop kwenye level nyngine, Ingawa bursts kutoka kwake inaonyesha kwamba alivutiwa na notorious. “ Nampenda Kanye West kwa hilo, kuwa producer, kufanya zile beats kali na rapper anafanya hivyo vyote ni mkali sana” alisema Ra. “ Nikiwa mahali alafu nikisikia ile ngoma yake ya “ Jesus walk” dah noma natulia nakuwa nataka mtu asinisumbue niisikilize ngoma hiyo ni kati ya ngoma zangu kali za Kanye West, haogopi kufanya ngoma ambazo zinavuka mipaka na kuongelea vitu ambavyo wasanii wengine wanaogopa kuimba” Alifunguka Rakim. Mwaka 2007 Rakim, Kanye West, Nas, KRS One na Dj Premier walishirikiana kwenye bonge moja la ngoma “Classic” katika kusherekea miaka 25 ya Nike Air force one sneaker.

No comments:

Post a Comment